Semina inasimamiwa na kituo cha mafunzo ya habari chini ya kitengo, kwa lengo la kuinua uwezo wa washiriki na kuboresha vipaji vyao.
Mmoja wa watumishi wa kituo Sayyid Muhammad Twawiil amesema “Kituo kimefanya semina ya upigaji wa picha kwa ugeni wa vijana ambao ni waandishi wa habari kutoka mkoa wa Waasit, mkufunzi alikua mmoja wa watumishi wa kitengo cha habari Sayyid Azharu Hamidi, amefundisha mbinu za upigaji wa pisha”.
Akaongeza kuwa “Semina imefanywa ndani ya ukumbi wa Qassim (a.s) katika Ataba tukufu, itadumu siku tano, kila siku watasoma saa tatu, wanafundishwa kwa nadhariya na vitendo”.
Semina hii ni sehemu ya ratiba maalum ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuimarisha uwezo wa vijana na vipaji vyao na kuwafanya waendane na maendeleo ya kisasa.