Kiongozi wa shamba boi Sayyid Hamidi Khadhiri Abbasi amesema “Watumishi wa vitalu vya Alkafeel wanaendelea kuvuna tende za msimu huu, wanavuna aina tofauti za tende kama vile Maktum, Mutwawwaq, Barihi, Khastawi, kutokana na kukaribia hatua ya mwisho hivi sasa wanavuna aina ya Zuhudi”.
Akaongeza kuwa “Baada ya mavuno, huanza kazi ya kuziweka kwenye vifungashio, kuzihifadhi na zingine kuingizwa sokoni”.
Akasisitiza kuwa “Mwaka huu tumepata tende nyingi tofauti na miaka ya nyuma, jambo ambalo litaongeza uwepo wetu katika soko la ndani”.