Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umeandaa na kutuma msaada wa kibinaadamu kwa raia wa Lebanon, kufuatia mashambulizi yanayofanywa katika nchi hiyo na utawala wa Izraeli.
Lifuatalo ni tamko la Ataba tukufu.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.
(Wale wanaosikiliza maneno na kufuata mazuri yake)
Katika kushikamana na raia wa Lebanon na kuwaliwaza kwa matatizo wanayopitia, sambamba na kutekeleza maelekezo ya Marjaa-Dini mkuu katika mji wa Najafu, yanayotaka waumini kusaidia raia wa Lebanon. Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umeandhaa shehena ya msada kwa raia wa Lebanon baada ya kuwasiliana na serikali ya Iraq, ili kuhakikisha msada huo unatumwa Lebanon haraka iwezekanavyo, Mwenyezi Mungu awalinde raia wa Lebanon, awaondolee shari na vitimbi vya waovu, awarehemu mashahidi wao na kuwaponya haraka majeruhi hakika yeye ni msikivu na mjuzi.