Kitengo cha maarifa kimetoa jarida la ishirini na sita la (Radu-Shamsi)

Hivi karibuni kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimechapisha toleo la ishirini na sita la jarida la (Radu-Shamsi).

Uchapaji wa jarida unasimamiwa na kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo.

Toleo hili limeandika tafiti za mambo muhimu katika historia ya Hilla, na limeandika utamaduni unaofatwa na watu tofauti katika jamii ya wakazi wa mji huo.

Jarida linapicha adimu za utamaduni wa wakazi wa mji wa Hilla na turathi zao, picha zinatoa uwelewa kamili wa mji huo kwa msomaji, sambamba na kugusia sekta ya Fiqhi, Adabu na Historia.

Jarida la (Radu-Shamsi) ni jarida la kitamaduni linalotegemewa na wanahabari wa Iraq, linawaandishi bora na wabobezi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: