Majmaa-Ilmi inaendelea na semina za kujenga uwezo kwa walimu wa kiislamu katika mkoa wa Diwaniyya.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya semina ya kuwajengea uwezo walimu wa kiislamu katika mkoa wa Diwaniyya kwa ushiriki wa walimu (30).

Semina inasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la wilaya ya Hamza chini ya Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu.

Washiriki wanafundishwa mbinu za ufundishaji, hukumu za tajwidi, visa vya Qur’ani, nafasi ya mwalimu katika kuandaa kizazi chema, malezi katika mtazamo wa Qur’ani na sunna na mengineyo.

Semina inadumu kwa muda wa siku nane chini ya wakufunzi waliobobea katika masomo ya Qur’ani na mbinu za ufundishaji.

Maahadi ya Qur’ani katika mkoa wa Najafu, imefanya awamu nne za semina kwa walimu wa mkoa wa Najafu, kwa lengo la kuboresha utamaduni wa kusoma Qur’ani na kutengeneza kizazi bora.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: