Kitengo cha maarifa kimechapisha kitabu kipya chenye anuani isemayo (Sherehe ya Nahjul-Balagha).

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimechapisha kitabu kipya chenye anuani isemayo (Sherehe ya Nahjul-Balagha), kutokana na uandishi wa Shekhe Hassan Matwar Khawibarawi aliyekufa mwaka 1410h.

Uchapishaji wa kitabu hicho umesimamiwa na kituo cha turathi za kusini chini ya kitengo.

Shekhe Khawibarawi aliandika kitabu hicho karne iliyopita, amesherehesha kwa ufupi kitabu cha (Nahjul-Balagha) kwa lengo la kufahamu kwa urahisi baadhi ya sentensi za kitabu hicho kitukufu.

Idara ya wahakiki katika kituo cha turathi za kusini, imehakiki sehemu iliyobaki ya kitabu hicho, kwani maandishi ya kitabu yamekaa bila kuchapishwa kwa muda unaokaribia nusu karne hadi baadhi yakapotea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: