Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kimesema kuwa, kiwango cha mafanikio katika mradi wa kituo cha Alkafeel kimefika asilimia 95.
Muhandisi mkazi Muhammad Fuadi amesema “Kituo cha uhawilishaji wa pili kilichojengwa na Atabatu Abbasiyya, kitakacho changia umeme kwa wakazi wa karibu na makaomakuu ya mji upande wa barabara ya Abbasi, kimefika mafanikio ya asilimia 95”.
Akaongeza kuwa “Kiwango cha uzalishaji wa kituo hico ni 31.5x2 (MVA), vifaa vyote vinavyotumika kwenye kituo vimetoka kwenye mashirika bora ya kimataifa”.
Kituo hicho kitasaidia kutoa huduma kwa wakazi wanaozunguka eleo hilo, kama vile barabara ya Abbasi, katikati ya mji na njia zinazoelekea Husseiniyya.