Maelfu ya mazuwaru wamemiminika katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mjini Karbala kuhuisha usiku wa Ijumaa.
Mji umeshuhudia idadi kubwa ya waumini waliokuja kufanya ziara katika Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya, ukiwa ni utamaduni wa wapenzi wa Ahlulbait (a.s).
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa huduma zote muhimu katika kurahisisha ufanyaji wa ziara kwa urahisi na utulivu.