Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amekagua utendaji wa shule za Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Ataba tukufu.
Ziara ya kiongozi mkuu wa kisheria katika sekta ya elimu inaonyesha jinsi anavyojali sekta hiuo, ukizingatia kuwa tupo mwanzoni mwa msimu wa mwaka mpya wa masomo.
Muheshimiwa Sayyid Swafi amekutana na rais wa kitengo cha malezi na elimu Dokta Hassan Daakhil na idara ya shule za wavulana na wasichana, amewahimiza kufanya kila wawezalo katika kuboresha sekta ya elimu na kupata matokeo bora.
Ziara hiyo imeonyesha wazi namna anavyojali sekta hiyo na imewashajihisha wanafunzi kusoma kwa bidii na kufikia malengo yao.