Kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimepokea ugeni kutoka Atabatu Alawiyya.
Mkuu wa kituo shekhe Mudriku Hasuun, amewaeleza wageni kuhusu utendaji wa kituo na namna kinavyo kusanya turathi za Basra na juhudi zake katika kuhuisha turathi hizo na kuzisambaza.
Rais wa ugeni huo Sayyid Hashim Muhammad Bajiji, ameeleza kuhusu jarida na machapisho yanayotolewa na Atabatu Alawiyya tukufu.
Shekhe Hasuun akakabidhi vitabu vilivyochapishwa na kituo kwa wageni, akawaomba wasaidie kuandika tafiti kuhusu turathi za Basra.