Sayyid Swafi ametoa ufafanuzi kuhusu shehena ya misaada iliyotolewa na Atabatu Abbasiyya kwa watu wa Lebanoni.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, ametoa maelezo kuhusu msaada wa kibinaadamu uliotolewa na Ataba tukufu kwa watu wa Lebanon, baada ya mashambulizi ya hivi karibuni.

Sayyid Swafi amesema kuwa wameunda kamati ya misaada, inayohusika kupeleka misaada kwa njia ya Aridhini kupitia Siriya, kamati hiyo itaweka kambi huko kwa ajili ya kusaidia wakimbizi wanaotoka Lebanon, huku kundi lingine la kamati hiyo litaweka kambi Bairuti kwa ajili ya kusaidia familia zitakazo athirika, sambamba na kuendelea kutuma shehena za misaada kwa kutumia ndege, kutoka Baghdad hadi Bairuti, tutatoa huduma za matibabu sehemu mbalimbali kwa haraka zaidi, akabainisha kuwa: Ataba tukufu itaweka vituo katika maeneo tofauti ya mji wa Karbala.

Atabatu Abbasiyya imetuma shehena ya misaada kwa raia wa Lebanon mara tu baada ya wito wa Marjaa-Dini mkuu wa kutoa huduma za kibinaadamu kwa wananchi wa Lebanon.

Akaongeza kuwa, vitu vinavyo tolewa na Atabatu Abbasiyya ni, chakula, dawa, mavazi, matandiko na mablangeti, kwa lengo la kusaidia wananchi wa Lebanon.

Akasema kuwa, milango iko wazi kwa kila mtu atakaependa kutoa mchango wake, chochote atakacho jaliwa mtu anaruhusiwa kutoa pesa au kitu, amana zote zitakazo pokelewa zitaingizwa kwenye orodha maalum na zitatangazwa, tayali tumesha tenga sehemu za kupokelea misaada na tumetoa namba za simu.

Kuhusu wanaotaka kushiriki katika utoaji wa huduma za afya, muhesimiwa kiongozi mkuu wa kisheria amesema, kwa kila anaependa kutoa kuduma za matibabu kwa majeruhi awasiliane na hispitali ya Alkafeel, ataandikishwa na kupewa nafasi ya kutoa huduma za afya wakati wa zowezi hili.

Mwisho wa maelezo yake, Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amemuomba Mwenyezi Mungu alilinde taifa la Lebanon na awaondolee wananchi wa taifa hilo mtuhani huu.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa namba za simu kwa ajili ya kukusanya misaada, sambamba na kutoa namba za kuwasiliana na viongozi wa kamati ya misaada, kwa lengo la kurahisisha ushiriki wa wananchi waliotayali kusaidia wananchi wa Lebanon katika mazingira haya magumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: