Atabatu Abbasiyya tukufu inajiandaa kupeleka msaada wa kitabibu nchini Lebanon, kupitia misafara yeke ya misaada kwa raia wa nchi hiyo baada ya shambulizi la hivi karibuni kufanywa na wazayuni.
Ataba tukufu ilianza kutuma misaada ya kibinaadamu baada ya Marjaa-Dini mkuu katika mji wa Najafu, kutoa wito wa kusaidia wananchi wa Lebanon.
Msafara unahusisha makumi ya tani za dawa na vifaa-tiba, vitafikishwa kwa waathirika nchini Lebanon kupitia serikali ya Iraq.
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa namba maalum kwa ajili ya kukusanya misaada, sambamba na kutoa namba za kuwasiliana moja kwa moja na wajumbe wa kamati ya kukusanya misaada, ili kurahisisha utoaji wa misaada kwa kila mtu atakaependa kufanya hivyo.