Atabatu Abbasiyya tukufu imetuma shehena ya kwanza ya misaada ya kibinaadamu kwa njia ya anga, ikiwa ni sehemu ya shehena za kusaidia wananchi ya Lebanon baada ya shambulio la mwisho nchini mwao kufanywa na Izrael.
Shehena inavitu mbalimbali pamoja na mambo ya kilojistik.
Shehena ya kwanza imeshindikizwa na ujumbe wa Ataba tukufu hadi uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Baghdad, kwa kushirikiana na serikali ya Iraq yenye jukumu la kufikisha msaada huo kwa waathirika nchini Lebanon.
Shehena hiyo itafuatiwa na shehena zingine, chini ya mkakati ulioandaliwa na kamati ya misaada iliyoundwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na serikali ya Iraq.
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa shehena ya misaada baada ya wito wa Marjaa-Dini mkuu katika mji wa Najafu, wa kusaidia wananchi wa Lebanon.
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa namba maalum kwa ajili ya kukusanya michango ya mali na imetoa namba za simu kwa ajili ya kuwasiliana na wajumbe wa kamati ya misaada moja kwa moja, ili kurahisisha ushiriki wa kila mtu anaetaka kutoa mchango wa kusaidia wananchi wa Lebanon katika wakati huu mgumu.