Atabatu Abbasiyya imeandaa shehena ya misaada baada ya Marjaa-Dini mkuu katika mji wa Najafu kutoa wito wa kusaidia wananchi wa Lebanon.
Imetoa nafasi kwa raia wanaopenda kuchangia, kwa kufungua vituo vya kupokelea misaada vinavyo simamiwa na kitengo cha Dini katika Ataba tukufu.
Atabatu Abbasiyya imeandaa namba maalum kwa ajili ya kukusanya michango na imetoa namba za kuwasiliana moja kwa moja na watu wa kamati ya misaada, ili kurahisisha ushiriki wa kila mtu anaependa kusaidia raia wa Lebanon katika wakati huu mgumu.