Kwa kuhudhuria viongozi wawili wa kisheria.. Ataba mbili zimefanya kikao cha kumsomea dua Sayyid Shahidi Hassan Nasrullah.

Uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya umefanya kikao cha kumsomea dua Hujjatul-islami wal-muslimina Sayyid Shahidi Hassan Nasrullah, wapiganaji wa Lebanon na wananchi waliouawa bila hatia.

Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi wakuu wa kisheria katika Ataba mbili Shekhe Abdulmahadi Karbalai na Sayyid Ahmadi Swafi pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Ataba mbili katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Hatua hii ni sehemu ya kuonyesha kushikamana kwetu na watu wa Lebanon katika mazingira magumu wanayo pitia ya kubomolewa nyumba zao na kuvunjwa kwa wazi haki za binaadamu.

Ofisi ya Muheshimiwa Marjaa-Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani, ilitoa tamko kufuatia kuuawa kwa Allamah Hujjatul-islami wal-muslimina Sayyid Hassan Nasrullah, sehemu ya tamko hilo inasema “Shahidi alikuwa kiongozi bora wa mfano, ni wachache sana watu kama yeye katika miongo ya hivi karibuni, amefanya kazi kubwa ya kuwashinda wavamizi wa Izrael na kukomboa ardhi ya Lebanon, alisaidia raia wa Iraq kwa hali na mali katika kukomboa miji iliyotekwa na magaidi wa Daesh, kama alivyo simama imara kusaidia watu wa Palestina, jambo lililopelekea kuuawa kwake”.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kukusanya misaada baada ya wito wa Marjaa-Dini mkuu katika mji wa Najafu, aliyetaka kusaidiwa raia wa Lebanon katika wakati huu mgumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: