Kiongozi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami amesema kuwa, Sayyid Shahidi Hassan Nasrullah amepata ushindi mkubwa uliokuwa haujawahi kupatikana kwa maadui wa Mwenyezi Mungu na ubinaadamu.
Ameyasema hayo alipohudhuria kikao cha dua kilichoandaliwa na uongozi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ya Allamah Hujjatul-islami wal-muslimina Sayyid Shahidi Hassan Nasrullah wapiganaji wa Lebanon na makumi ya wananchi waliouawa bila hatia.
Amesema: “Mwenyezi Mungu mtukufu humuwafikisha muuminu hapa duniani na humkirimu kwa kumpa kilele cha utukufu nayo ni shahada, ambayo ameipata Sayyid Hassan Nasrullah baada ya kazi kubwa ya jihadi aliyofanya umri wake wote, katika kazi hiyo amepata ushindi mkubwa dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu na ubinaadamu”.
Akaongeza kuwa “Kikao cha dua kimefanywa kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, ni sehemu ndogo ya kuonyesha kuumizwa kwetu na kuuawa kwa mtu huyu mtukufu sambamba na kupeana pole kwa msiba huu mkubwa”.
Kikao cha kuomboleza kimeanza siku ya Jumapili 25 Rabiul-Awwal 1446h, sawa na 29/9/2024m saa tisa jioni na kitaendelea kwa muda wa siku tatu katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.