Kundi kubwa la waumini linashindikiza jeneza la igizo la Allamah Hujjatul-islami wal-muslimina Sayyid Shahidi Hassan Nasrullah mbele ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Wameshiriki viongozi wa kidini, kijamii na mazuwaru katika kushindikiza jeneza hilo.
Matembezi ya kushindikiza jeneza yameanzia ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), jeneza limebebwa katika mazingira yaliyojaa huzuni na majonzi, wakaelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kufanywa vikao vya uombolezaji ambapo matamko mbalimbali yametolewa na kueleza utukufu wa Shahidi na kujitolea kwake.
Ataba mbili tukufu zilikua zimeshafanya kikao cha kumsomea dua Allah Sayyid Shahidi Hassan Nasrullah, wapiganaji wa Lebanon na makumi ya raia waliouawa, mbele ya viongozi wakuu wa kisheria katika Ataba mbili tukufu, Shekhe Abdulmahadi Karbalai na Sayyid Ahmadi Swafi kwenye eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Hatua hii ni sehemu ya kuonyesha kushikamana na watu wa Lebanon katika mashambulizi ya kinyama yanayofanywa kwenye makazi yao na uvunjwaji wa haki za binaadamu wa wazi.