Atabatu Abbasiyya tukufu: Tunaendelea kukusanya misaada na kuituma kwa watu wa Lebanon

Atabatu Abbasiyya tukufu imesisitiza kuwa, inaendelea kukusanya misaada na kuituma kwa watu wa Lebanon ikiwa ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa-Dini mkuu.

Mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhammad Ashqar amesema, Hakika Ataba tukufu kwa kushirikiana na wahisani miongoni mwa waumini, inakusanya michango tofauti, ikiwa ni pamoja na nafaka za chakula kavu na mbichi, akasisitiza kuwa “Kipaombele ni maziwa ya watoto na nafaka kuu za chakula kutokana na udharura wa watu wa Lebanon”.

Akafafanua kuwa “Shehena ya misaada imeondoka na inatarajia kufika kwa wahitaji wa Lebanon na Sirya sambamba na kusaidia wakimbizi waliopo makambili na wale watakaokuja Iraq”.

Akaendelea kusema “Tumeandaa vifaa-tiba na dawa kwa ajili ya kutibu majeruhi na wagonjwa, shehena hiyo itatumwa kwa wahitaji pia”, akabainisha kuwa “Atabatu Abbasiyya imeandaa kamati maalum chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, kuna kamati ya kukusanya michango ya vitu, michango ya pesa na kamati maalum ya kutembelea wakimbizi wa Lebanon na Sirya kwa ajili ya kutathmini mahitaji yao”.

Akaendelea kusema, kufuatia mkakati wa kusaidia wakimbizi waliokatika mazingira magumu, wale wanaolala barabarani, Atabatu Abbasiyya imekusanya kiwango kikubwa cha vifaa vya kulalia na vitatumwa katika sheheza ya misaada.

Akasema kuwa vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya vinasaidia kuratibu na kutunza misaada, akasisitiza kuwa Atabatu Abbasiyya itaendelea kutoa misaada ya kibinaadamu na kushikamana na watu wa Lebanon katika mazingira haya magumu, itafanya kila iwezalo katika kupunguza matatizo wanayopatia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: