Ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria ya mambo ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya majlisi ya kumuomboleza Allamah Sayyid Hassan Nasrullah na wapiganaji wa Lebanon.
Majlisi ya kwanza imefanywa asubuhi katika kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s) na majlisi ya pili imefanywa jioni katika Sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a,s) ndani ya haram tukufu.
Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ikafuata tenzi na qaswida za kuomboleza kwa ushiriki wa idara za wanawake chini ya Ataba tukufu.