Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu nchini Siria, umetembelea majeruhi wa Lebanon waliolazwa kwenye hospitali za nchi hiyo.
Mmoja wa ujumbe huo Shekhe Haidari Aaridhwi amesema “Ujumbe wa Ataba tukufu umetembelea majeruhi kutoka Lebanon waliolazwa katika hospitali za Siria na kuangalia mahitaji yao pamoja na kuongea na uongozi wa hospitali kuhusu hali zao kiafya”.
Akaongeza kuwa “Ujumbe umegawa zawadi za kutabaruku na Abulfadhil Abbasi (a.s) na misaada mingine kwa wagonjwa, jambo hilo linaonyesha kusimama pamoja na watu wa Lebanon”.
Akaendelea kusema “Jambo hilo linaonyesha kushikamana na ndugu zetu wananchi wa Lebanon wanaoshambuliwa na mazayuni”.
Atabatu Abbasiyya tukufu inatuma misaada ya kibinaadamu nchini Lebanon, kuitikia wito wa Marjaa-Dini mkuu katika mji wa Najafu, kupunguza machungu ya watu wa Lebanon wanayopitia kutokana na mashambulizi ya mazayuni.