Atabatu Abbasiyya imefika kituo cha mbali zaidi sehemu ya mpakani baina ya Siria na Lebanon kwa ajili ya kusaidia wakimbizi

Idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya imesema kuwa kikosi chake kimefika kwenye mpaka wa Siria na Lebanon kutoa huduma za kibinaadamu kwa familia za wakimbizi.

Kiongozi wa Idara Shekhe Haidari Aaridhi amesema “Hatua hiyo ni kuitikia wito wa Marjaa-Dini mkuu Sayyid Ali Hussein Sistani, aliyetoa tamko la kusaidia wananchi wa Lebanon, katika utekelezaji wa tamko hilo Atabatu Abbasiyya imetuma misafara mingi yenye shehena za misaada ya kibinaadamu kwa wakimbizi”.

Akaongeza kuwa “Kikosi cha watumishi wa ustawi wa jamii kimefika sehemu ya mbali zaidi kwenye mpaka wa Siria na Lebanon, kimepokea familia za wakimbizi na kuwafikishia salamu za Muheshimiwa Sayyid Ali Sistani na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi”.

Akasema kuwa “Ziara hiyo inalenga kutoa misaada kwa familia za wahanga wa vita, ikiwemo misaada ya kipesa huku wakisubiri misaada mingine kutoka mji wa Imamu Hussein (a.s) katika maeneo hayo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: