Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya nchini Siria, umefungua hospitali maalum kwa ajili ya kutibu majeruhi kutoka Lebanon wanaokimbilia nchini humo.
Kiongozi wa ujumbe wa Ataba Sayyid Naafii Mussawi amesema “Ujumbe umefungua hospitali maalum yenye madaktari wengi kwa ajili ya kutibu watu wanaojeruhiwa kutokana na mashambulizi ya mazayuni nchini Lebanon”.
Akaongeza kuwa “Ufunguzi wa hospitali hiyo ni matokea ya shehena za misaada zinayotumwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa watu wa Lebanon, ambapo misaada hiyo inahusisha vifaa-tiba, jopo la madaktari, wauguzi, gari za wagonjwa na dawa”.
Atabatu Abbasiyya imeanza kutuma shehena za misaada baada ya wito wa Marjaa-Dini mkuu Ali Husseini Sistani, wa kutaka kusaidiwa watu wa Lebanon kufuatia mashambulizi yanayofanywa na mazayuni katika nchi hiyo.