Ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya umeanza kugawa chakula kwa wakimbizi wa Lebanon nchini Siria.

Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya nchini Siria, umeanza kugawa chakula kwa wakimbizi wa Lebanon, kutokana na mashambulizi ya mazayuni mchini kwao.

Kiongozi wa ujumbe huo Sayyid Naafii Ni’mah Mussawi amesema “Ujumbe kutoka Ataba tukufu, umeanza kugawa chakula kwa wakimbizi wa Lebanon nchini Siria milo mitatu kila siku, kupitia jiko maalum lililoanzishwa kwa ajili ya jukumu hilo”.

Akaongeza kuwa “Ujumbe wetu kwa kushirikiana na ofisi ya Marjaa-Dini nchini Siria, umetenga sehemu mbili, sehemu ya jiko ipo karibu na haram ya Bibi Zainabu (a.s) na sehemu ya kupokelea shehena za misaada kutoka Iraq, ambapo pia nafaka za chakula zinatolewa kwa familia za wahanga”.

Shughuli zote zinafanywa chini ya utaratibu maalum uliowekwa na Atabatu Abbasiyya, ikiwa ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: