Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Sayyid Shahidi Hassan Nasrullah nchini Pakistani

Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Sayyid Shahidi Hassan Nasrullah nchini Pakistani.

Muwakilishi wa Ataba tukufu katika nchi ya Pakistani Shekhe Naaswir Abbasi Najafi amesema “Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Muheshimiwa Hujjatul-Islami wal-muslimina Sayyid Shahidi Hassan Nasrullah na mashahidi aliouawa pamoja nao, katika mkoa wa Jakwali mji wa Panjab nchini Pakistani”.

Akaongeza kuwa “Majlisi imeandaliwa na wanafunzi wa Dini katika mkoa huo, imehudhuriwa na muwakilishi wa Marjaa (Mu’utamad Marjaiyya), wakuu wa shile za kidini, maimamu wa misikiti na kundi kubwa la waumini, katika majlisi hiyo limesomwa tamko la Marjaa-Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani kufuatia kuuawa kishahidi kwa Sayyid Nasrullah”.

Majlisi hiyo inaonyesha kuchukizwa na jinai hiyo, pamoja na kuungana kikamilifu na watu wa Lebanon katika wakati huu mgumu wa kushambuliwa nchi yao na kuvunjwa kwa haki za binaadamu katika taifa lao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: