Majmaa-Ilmi imefanya semina ya Qur’ani katika fani ya sauti na naghma za mahadhi ya kimisri.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya semina ya Qur’ani, imejikita katika kuboresha vipaji vya sauti na naghma katika usomaji wa kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa mahadhi ya kimisri.

Semina imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu ikiwa na washiriki (20).

Kiongozi wa idara ya usomaji Sayyid Ahmadi Zaamili amesema “Mkufunzi wa semina alikuwa ni msomaji Alaa Swadiqi, amefundisha mambo tofauti yanayohusu fani ya sauti na naghma, amefafanua kwa kina kuhusu maqamaat yanayotumiwa na msomaji kuboresha sauti wakati wa kusoma Qur’ani”.

Akaongeza kuwa “Semina imekuwa na kipengele cha mazowezi ya sauti na naghma kwa lengo la kuboresha uwezo wa kusoma Qur’ani, itakuwa inafanyika mara mbili kwa wiki ndani ya miezi mitatu”.

Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu, hufanya semina za Qur’ani kipindi chote cha mwaka, hufundisha usomaji sahihi na hukumu za tajwidi, imesha toa mamia ya wahitimu wanaoendelea kufundisha Qur’ani katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: