Atabatu Abbasiyya imefanya kongamano la idara zinazoshuriki kukusanya misaada ya watu wa Lebanon

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umefanya kongamano la idara zinazoshiriki kukusanya misaada ya watu wa Lebanon.

Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Maitham Zaidi amesema “Kongamano la idara zinazoshiriki kukusanya michango ya kusaidia watu wa Lebanon, chakula, dawa na vitu vingine, kutoka mikoa tofauti ya Iraq, chini ya maelekezo ya katibu mkuu wa Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa “Kongamano limehusisha utoaji wa tuzo kwa mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami, kutoka kwa muwakilishi wa idara zinazoitikia wito wa Marjaa-Dini mkuu na zinashirikiana na Atabatu Abbasiyya katika kukusanya misaada ya watu wa Lebanon”.

Akasisitiza kuwa “Kongamano limesisitiza umuhimu wa kushirikiana katika kukusanya misaada kwa kiwango kinachoendana na matatizo wanayopitia watu wa Lebanon sambamba na kuratibu misafara ya shehena za misaada”.

Atabatu Abbasiyya imeshatuma misafara mitatu ya shehena za misaada, msafanya mmoja umepelekwa kwa njia ya anga na miwili kwa njia ya barabara, zaidi ya tani 1300 za chakula, dawa na vifaa vingine zimetumwa Siria kwa ajili ya kusaidia wakimbizi wa Lebanon pamoja na kufungua jiko kubwa la kupika na kugawa chakula kwa wakimbizi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: