Idara ya Tablighi katika Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya kwanza.
Majlisi imefanywa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na imehudhuriwa na Sayyid Hassan Mussawi, itadumu kwa muda wa siku tatu.
Majlisi imepambwa na mada mbalimbali, zikiwemo zinazomuhusu Bibi Zaharaa (a.s), historia yake, elimu yake, ufasaha wake, hekima zake, nafasi yake mbele ya Mtume (s.a.w.w) na subira yake katika wakati mgumu wa kulinda bendera ya Utume na Uimamu.
Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya majlisi maalum zinazohusu watu wa nyumba ya Mtume (a.s), kwa lengo la kuhuisha utajo wao na kusambaza elimu zao.