Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imefanya mahafali ya kuadhimisha kuhitimu wanafunzi 300 wa semina za hukumu za usomaji wa Qur’ani.
Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema “Maahadi imefanya mahafali ya wahitimu 300 wa semina za hukumu za usomaji wa Qur’ani, iliyodumu kwa muda wa miezi sita”, akaongeza kuwa “Maahadi iliandaa maswali ya kujibu kwa kuandika na kuongea, wanafunzi wamefaulu kwa kiwango kikubwa”.
Aljaburi amebainisha kuwa “Mahafali ilikuwa na vipengele tofauti, kikiwemo cha kusoma aya za Qur’ani kwa sauti ya msomaji Jamana Abduridhwa na usomaji wa pamoja wakikundi cha Nab’ul-Juud chini ya Maahadi”.
Akafafanua kuwa “Vipengele vya mahafali vimepambwa na qaswida kutoka kwa kikosi cha mabinti wa Raudha ya Ahbaabul-Kafeel na maswali yanayohusu Qur’ani”, akasema kuwa “Mahafali imeshuhudia utoaji wa vyeti na zawadi kwa washiriki, ikiwa ni sehemu ya kuwashajihisha waendelee na kuhifadhi Qur’ani tukufu na kusambaza utamaduni wa kuisoma”.