Kupitia idara za ustawi wa jamii.. Atabatu Abbasiyya inaendelea kukusanya misaada ya watu wa Lebanon

Idara za ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya tukufu, zinaendelea kukusanya misaada ya chakula kwa watu wa Lenanon kupitia vituo vyake vya mikoani.

Mmoja wa watumishi wa idara Sayyid Yaasir Aqiil amesema “Idara za ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya zinaendelea kukusanya misaada ya nafaka za chakula mikoani, kuna jumla ya vituo 19 katika maeneo tofauti.

Akaongeza kuwa “Idara zinajukumu la kukusanya misaada kutoka kwa watu binafsi na mawakibu husseiniyya, kisha hutumwa Majmaa-Alqami halafu hupelekwa kwenye maghala ya Atabatu Abbasiyya ambako hufanyiwa uchambuzi na kupakiwa kwenye shehena kwa ajili ya kusafilishwa na kupelekwa kwa watu wa Lebanon na familia za wakimbizi waliopo Siria”.

Jambo hilo ni sehemu ya juhudi za kibinaadamu zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, katika kupunguza maumivu wanayopitia watu wa Lebanon kutokana na kushambuliwa na mazayuni, aidha ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa-Dini mkuu katika mji wa Najafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: