Ugeni kutoka ubalozi wa Japani umesifu kazi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya ya kusaidia watu wa Lebanon.

Ugeni kutoka ubalozi wa Japani umepongeza kazi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kusaidia watu wa Lebanon.

Wametoa pongezi hizo baada ya kutembelea baadhi ya miradi na harakati za kibinaadamu zinazofanywa kwa ajili ya kusaidia watu wa Lebanon kutokana na kushambuliwa kwao na mazayuni.

Rais wa ugeni huo Muheshimiwa Mikau amesema “Atabatu Abbasiyya inatoa msaada ya kibinaadamu kwa watu wa Lebanon waathirika wa vita waliopo nchini humo na waliokimbilia Siria”.

Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya inafanya kazi kubwa za kidini na kijamii”.

Akasema “Nimefurahishwa na miradi ya Atabatu Abbasiyya katika sekta ya afya, kilimo na ujenzi pamoja na miradi mingine inayolenga kuhudumia jamii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: