Kitengo cha habari na utamaduni kimetoa mihadhara ya kielimu kwa wageni kutoka Dhiqaar.

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimetoa muhadhara kwa wageni kutoka mkoa wa Dhiqaar.

Mmoja wa wajumbe wa kituo cha Multaqal-Qamaru chini ya kitengo Sayyid Adbullahi Jabbaar amesema “Tumepokea ugeni wa kisekula unaojumuisha walezi na walimu kutoka mkoa wa Dhiqaar, tumewapa mihadhara ya kitamaduni na kidini, tumebainisha mafundisho ya kimalezi kwa walimu”.

Akaongeza kuwa “Mazingira tofauti yanayokumba jamii ya raia wa Iraq, yanahitaji kufundishana misingi ya kimalezi na kimaadili, kwa ajili ya kunufaisha vijana na kurekebisha fikra zao kwa kuziongoza katika mambo ya kimaadili”.

Muwakilishi wa wageni Sayyid Haidari Abduridhwa, amepongeza mapokezi na huduma nzuri walizopewa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kituo cha Multaqal-Qamaru kinapokea wageni mbalimbali kutoka mikoa yote ya Iraq, chini ya ratiba maalum inayolenga kujenga misingi ya kitamaduni na kidini, sambamba na kufanya warsha na semina.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: