Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya ametembelea shule za Al-Ameed

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini ametembelea shule za Al-Ameed zilizochini ya Ataba tukufu.

Amepokewa na rais wa kitengo cha malezi na elimu katika Ataba, Dokta Hassan Daakhil na makamo wake Sayyid Yusufu Twaaiy na baadhi ya viongozi.

Muheshimiwa katibu mkuu amekagua maendeleo ya kielimu na kimalezi katika shule za Al-Ameed na amesikiliza maelezo kuhusu mikakati ya kielimu ya mwaka huu.

Akasisitiza umuhimu wa taasisi za elimu katika Atabatu Abbasiyya na nafasi yake katika kuendeleza sekta ya elimu.

Muheshimiwa katibu mkuu amepongeza maandalizi mazuri ya shule hizo yanayo endana na maendeleo ya kielimu na kiteknolojia.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya amesifu kazi nzuri inayofanywa na walimu, amewataka waendelee kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kujituma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: