Atabatu Abbasiyya imepokea zaidi ya watu 1000 kutoka Lebanon miongoni mwa wageni wa Iraq.

Kamati inayohusika na malazi katika Atabatu Abbasiyya, imesema kuwa imepokea zaidi ya watu 1000 kutoka Lebanon miongoni mwa wageni wa Iraq na wamepewa huduma tofauti.

Mjumbe wa kamati Sayyid Muhammad Ali Azhar amesema “Kamati imepokea zaidi ya watu 1000 kutoka Lebanon, imewapa sehemu za kulala, hoteli nne na majengo mengine ya kutolea huduma sambamba na kuandaa nyumba kadhaa”.

Akaongeza kuwa “Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya, kimesimamia mapokezi na kuandaa makazi yao huku kitengo cha mgahawa (mudhifu) kikisimamia ugawaji wa chakula kwa wageni hao kinawapa milo mitatu kila siku”.

Akabainisha kuwa “Sehemu za malazi zinavifaa vyote muhimu, jambo hili ni sehemu ya huduma zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa raia wa Lebanon”.

Akasema kuwa “Miongoni mwa huduma wanazopewa ni pamoja na matibabu katika hospitali ya rufaa Alkafeel na vituo vya afya vilivyo andaliwa sehemu za makazi yao, sambamba na kuwapa misaada ya pesa za kujikimu na mambo mengine wanayohitajia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: