Idara ya Fatuma binti Asadi ya masomo ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea kufundisha (Naghma za Qur’ani) kwa wapenzi wa Que’ani.
Semina inahusisha masomo mengi, wanafundisha kwa nadharia na vitendo na sasahivi ni wiki ya tatu mfululizo.
Semina inamada tofauti, miongoni mwa mada zake ni: Aina za sauti, kutambulisha maqamaat (mahadhi), pamoja na kufanya baadhi ya vitendo vinavyo endana na masomo hayo, na kutambua namna ya kunufaika nayo.
Idara hufanya harakati mbalimbali zinazohusu Qur’ani.




