Kituo cha utamaduni wa familia kimeandaa program ya wanafunzi wa chuo jijini Baghdad.

Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya kimeandaa program yenye anuani isemayo “Korido ya utamaduni” kwa watumishi wa chuo cha teknolojia na wanafunzi wake mkoani Baghdad.

Program inafanywa kwa kushirikiana na kitengo cha wanawake katika taasisi ya wafungwa wa kisiasa, muhadhara wenye anuani isemayo “Mwanaadamu baina ya uhuru na utumwa” imewasilishwa na Dokta Shaimaa Nasoro, ameongea kuhusu uwelewa wa uhuru na athari yake katika maisha ya mtu na jamii”.

Bibi Fatuma Zainudini ametoa zowezi lililojikita katika hisia mbaya kiafya, ili kusaidia washiriki waweze kujitambua na akahitimisha kwa kuuliza maswali ya kifiqhi, kipengele hicho kikaongozwa na Bibi Ikhlasi Jawaad.

Program hiyo ni sehemu ya harakati za kituo kwa jamii ya wanawake, iyolenga kuwawezesha kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: