Idara ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imetoa muhadhara wa kimalezi kwa wageni kutoka shule za wasichana za Tawareji.
Kiongozi wa idara Bibi Adharaa Shami amesema “Kutokana na umuhimu wa mwanamke katika kujenga jamii na kujenga familia, tumetoa mihadhara ya kimalezi yenye mada tofauti kulingana na umuhimu wa mwanamke katika maisha, sambamba na kujadili uwelewa wa kujistiri katika sheria ya kiislamu”.
Akaongeza kuwa “Muhadhara umetolewa kwa wanafunzi wa shule za Towareji, ambapo imeelezwa maana ya stara kuwa ni ngao inayolinda na kutunza heshima ya mwanamke katika jamii”.
Wanafunzi wamepongeza kazi kubwa inayofanywa na idara ya Dini katika kuhudumia jamii ya wanawake na kuhuisha turathi za Ahlulbait (a.s).
