Hivi karibuni kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimechapisha kitabu kiitwacho (Mwenye mbawa mbili Jafari).
Kitabu hicho ni sehemu ya uandishi wa Shekhe Abduzahara Swaghiir, kinaeleza historia ya Jafari bun Abu Twalib, ushujaa wake, kujitolea kwake na kuuawa kwake kishahidi, kutoka katika vyanzo vikubwa vinne vinavyo taja utukufu wa Jafari bun Abu Twalib vilivyo andikwa na Abu Hassan Madaaini, Abu Ahmadi Abdul-Azizi bun Yahaya Jaludi, Shekhe Swaduqu na Dhiyaau-Dini Almaqdasi.
Nacho ni kitabu cha pekee, kwa sababu Shekhe Swaghiir hakutumia kitabu chochote miongoni mwa vitabu vya kisasa, bali katumia vitabu vya zamani ambavyo havijachapishwa kisasa, kitabu hicho kimehakikiwa na kituo cha turathi za kusini na kukidhi vigezo vya turathi halisi za kiislamu.
Kituo cha turathi za kusini kinafanya kazi kubwa ya kuhuisha turathi za kiislamu kutoka mikoa tofauti, ukiwemo mkoa wa Dhiqaar, Misaan, Qadisiyya na Muthanna.