Majmaa-Ilmi katika Atabatu Abbasiyya imefanya kikao cha usomaji wa Qur’ani kwa lengo la kuandaa wasomaji bora.
Kikao hicho kimesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.
Sayyid Ali Zubaidi kutoka idara ya usomaji amesema “Kikao kimefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha washiriki wakaanza kusoma na kupokea maoini na maelekezo kutoka kwa mwalimu anaesimamia kikao hicho, Shekhe Mahadi Qalandari, ambaye anaangalia hukumu za usomaji, kusimama, kuanza, sauti na naghma”.
Akaongeza kuwa “Kikao kilikuwa na muhadhara usemao (Nani msomaji?) wametambulishwa wasomaji watatu, ukatengwa muda wa kumsikiliza msomaji mmoja wa kimataifa”.
Akaendelea kusema “Kikao kilichofanywa katika ofisi za Maahadi ya Qur’ani mjini Najafu kimekamilika kwa kufanya shindano la Qur’ani, lililokuwa na maswali tofauti kuhusu maudhui za Qur’ani, Akhlaq, Fiqhi na Aqida, washiriki wamejibu maswali kupitia program ambayo majibu yao yalionyeshwa moja kwa moja kwenye kioo cha luninga”.





