Kitengo cha habari na utamaduni kinafanya semina ya kufundisha mfumo wa kimataifa RDA kwa watumishi wa Majmaa-Ilmi

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa semina ya kufundisha mfumo wa kimataifa RDA kwa watumishi wa Majmaa-Ilimi wa Iraq.

Sayyid Ali Twalibu kutoka kituo cha faharasi na mpangilio wa taaluma chini ya kitengo amesema “Idara ya faharasi katika kituo, imeandaa semina ya faharasi za nakala-kale kwa kufuata mfumo wa kimataifa RDA na Mark21 kwa watumishi wa Majmaa-Ilmi wa Iraq.

Akaongeza kuwa “Semina itadumu kwa siku tano, wanafundishwa kwa nadharia na vitendo, sambamba na kutumia program ya (Huka) iliyotengenezwa hivi karibuni na watumishi wa kituo cha faharasi”.

Kiongozi wa idara ya majalada na majarida katika Majmaa Sayyid Raaid Jaasim Mussawi amesema “Semina inabainisha namna ya kuandaa faharasi za nakala-kale na kuziweka kwa namba, inafaida kubwa kwa watumishi wetu”, ameshukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuandaa semina hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: