watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram wanapanga vitabu vya dua na ziara ndani ya Atanatu Abbasiyya

watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanapanga vitabu vya dua na ziara ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati wote.

Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Zainul-Aabidina Quraishi amesema “Watumishi wa idara ya vitabu chini ya kitengo, wanafanya kazi ya kupanga vitabu vya dua na ziara vilivyopo ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kengo la kuangalia usalama wake na kuendelea kutumiwa na mazuwaru wakati wote”.

Akaongeza kuwa “Kazi hiyo inahusisha ukarabati wa vitabu vilivyo haribika na kupangilia vizuri karatasi zake chini ya usimamizi wa kikosi bobezi katika fani hiyo”.

Kitengo cha usimamizi wa haram katika Atabatu Abbasiyya kinatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wa malalo ya mwezi wa familia (a.s) na kuwarahisishia ufanyaji wa ziara ndani ya malalo takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: