Kitengo cha Dini kinaendelea kutoa mihadhara ya kifiqhi ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kinafanya mihadhara ya kifiqhi na kiaqida ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Rais wa kitengo shekhe Swalahu Karbalai amesema “Mihadhara ya kidini inatolewa katika wakati muwafaka karibu na swala ya Adhuhuri ili kuweka mazingatio kwa waumini, huongelewa mambo muhimu katika maisha ya watu”.

Akaongeza kuwa “Mihadhara inajikita katika kueleza misingi mikuu ya Fiqhi, kama vile kufafanua kitabu cha Masaailu-Muntakhaba, mambo ya Muamalaati kama vile, kuuza, kununua, kupanga na mengineyo, sambamba na kufafanua mambo ya haramu katika sheria ya kiislamu na namna ya kujiepusha nayo”.

Akaendelea kusema “Muhadhara wa leo umeelezea swala, ambayo ni miongoni mwa wajibu muhimu zaidi baada ya Aqida, umebainisha masharti ya mwenye kuswali na sehemu ya kuswalia pamoja na kuongea mambo ya kimaadili na kijamii”.

Ratiba hiyo ni sehemu ya harakati za kitengo cha Dini katika kujenga uelewa wa mambo ya kifiqhi na kimaadili kwa mazuwaru wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kuimarisha unyenyekevu wa kiroho unaohitajika katika maisha ya kila siku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: