Kitengo cha maarifa kinashiriki kwenye maonyesho ya vitabu katika chuo kikuu cha Basra.

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chini ya Atabatu Abbasiyya, kimeshiriki kwenye maonyesho ya vitabu katika chuo kikuu cha Basra.

Maonyesho yameandaliwa na Daaru-Fihaau ya uchapaji na usambazaji wa vitabu, ndani ya ukumbi wa maktaba ya chuo kikuu cha Basra kwa kushirikiana na uongozi mkuu wa maktaba hiyo.

Kitengo kimeshiriki kupitia tawi maalum lililo onyesha machapisho yaliyotolewa na kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo, ambayo ni majarida na vitabu vyenye anuani za adabu, historia, fikra, turathi, fiqhi, tafsiri, hadithi na aina zingine mbalimbali.

Ushiriki wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya ni kwa ajili ya kuimarisha mahusiano na taasisi mbalimbali za kielimu, hususan kwenye sekta ya utamaduni pamoja na kutambulisha machapisho yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: