Hivi karibuni kitengo cha Maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimechapisha kitabu kipya chenye anuani isemayo: (Muqadimatu kitabu rijaali fi mabadiu ilmu rijaali).
Uchapishwaji wa kitabu hicho umesimamiwa na kituo cha turathi za kiislamu katika mji wa Mashhad tukufu chini ya kitengo, nacho ni miongoni mwa uandishi wa Sayyid Mirza Muhammad Ali Mudarisi Radhwawiyyu.
Kitabu kinakurasa 150, kimeandika changamoto zote na shubuha zenye manufaa zilizozushwa katika ilmu-rijaali na watu wa Akhbariyuna, amejibu shubha (utata) kwa maelezo ya kina.
Kitabu kinaonyesha, muandishi anauwezo mkubwa wa kufikiri na uzowefu wa muda mrefu katika kujibu shubuha za ilmu-rijaali, ameandika hoja za wanaopinga ilmu-rijaali kisha akazijibu na kuonyesha ulazima wa kuhitajika kwa ilmu-rijaali.
Muandishi ametumia vitabu vya usulu na kanuni za usulu, kitabu hicho kimehakikiwa na kituo tajwa, kutokana na umuhimu wa ilmu-rijaali katika mambo mengi ya kidini.
