Mkuu wa kitengo cha usajili wa wanafunzi Sayyid Ahmadi Yakob amefafanua kuwa “Usajili unahusisha kufungua mitandao ya wanafunzi kwenye jukwaa la masomo kwa njia ya mtandao, na kuthibitisha taarifa zao kisha wanachagua kitivo kwa kuzingatia vigezo vya chuo”.
Akasema kuwa “Chuo kimeandaa mambo yote ya logistic (huduma muhimu za kibinaadamu), sambamba na kuandaa kikosi maalum kwa ajili ya kujibu maswali ya wanafunzi na kuwapa maelekezo, wanafunzi waliokubaliwa kujiunga na chuo wanapewa vitambulisho vya chuo wanavyo takiwa kuonyesha getini wakati wa kuingia na kutoka”.
Chuo kikuu cha Al-Ameed kimeandaa mazingira bora ya masomo, kuanzia kumbi za madarasa, maabara, vifaa vya kusomea vya kisasa vinavyo mrahisishia mwanafunzi katika usomaji.




