Atabatu Abbasiyya tukufu imeadhimisha mazazi ya Bibi Zainabu (a.s) kwa kufanya hafla katika vitalu vya Alkafeel.
Kiongozi wa eneo hilo Sayyid Muhammad Harbi amesema “Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia ratiba ya hafla zake kwenye maeneo tofauti, imefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya Bibi Zainabu (a.s) katika vitalu vya Alkafeel”.
Akaongeza kuwa “Hafla imepambwa na kipengele cha mashairi kutoka kwa kikosi cha washairi na waimbaji, mbele ya kundi kubwa la familia za watu wa Karbala, wamegawa maua kwa wahudhuriaji”.
Akafafanua kuwa “Atabatu Abbasiyya tukufu huadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s)”.
Sayyid Muhammad Kadhim kiongozi wa idara ya mawasiliano katika kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya amesema “Hafla ilikuwa na vipengele vingi vinavyo endana na tukio hilo, imefanywa kwa kushirikiana na vitengo tofauti vya Atabatu Abbasiyya tukufu”.






