Wakati wakupokea wageni kutoka Madakaska.. Sayyid Swafi amesisitiza utayali wa Atabatu Abbasiyya kutoa msaada wa kitamaduni kwa waumini katika nchi tofauti.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amesema kuwa, Ataba ikotayali kutoa misaada ya kitamaduni kwa waumini wa nchi tofauti za Afrika kama itakavyo wezekana.

Ameyasema hayo mbele ya wageni wa kidini na kitamaduni kutoka nchini Madagaska, sambamba na kusikiliza hali ya waumini wa nchi hiyo na mahitaji yao.

Katika mazungumzo yake akaashiria kuwa Atabatu Abbasiyya iko tayali kusaidia sekta ya utamaduni kwa waumini wa nchi tofauti kama itakavyo wezekana.

Akasisitiza kuwa Atabatu Abbasiyya ikotayali kupokea wanafunzi wa kisekula kutoka kwenye nchi hizo, kuja kusoma katika chuo kikuu cha Al-Ameed na Alkafeel, chini ya masharti ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu ya Iraq.

Rais wa kitengo cha mahusiano ya kidini na kitamaduni nchini Madagaska na Afrika Sayyid Ridhwa Lahiriji amesema, wageni wamekutana na Muheshimiwa Sayyid Swafi, wamesikiliza nasaha zake, wamekubaliana kutuma vijana kutoka Afrika watakaokuja kujiunga na chuo kikuu cha Al-Ameed na Alkafeel, ili watakapo rejea waweze kutumikia Dini yao na mataifa yao.

Akasisitiza kuwa Ataba tukufu inaushirikiano mzuri kwenye sekta mbalimbali, wageni wameshukuru sana watendaji wa Ataba tukufu kwa mapokezi mazuri na huduma bora.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: