Kitengo cha maadhimisho kinaendelea na maandalizi ya kuhuisha maombolezo ya Fatwimiyyu.

Kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya kinafanya maandalizi ya maombolezo ya Fatwimiyyu, kwa ushiriki wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya vya Karbala.

Makamo rais wa kitengo Sayyid Ahmadi Shakiri Mussawi amesema “Kitengo cha maadhimisho kinaendelea na maandalizi ya kuhuisha huzuni za Fatwimiyyu, yamehusisha ujenzi wa nyumba ya huzuni (baitul-ahzaan) katika eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili, sambamba na kuweka baadhi ya vipengele vinavyo eleza historia ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Maandalizi yanafanywa kwa kushirikiana na kikosi cha Abbasi (a.s), Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya vya Karbala, kitengo kimeandaa sehemu maalum kwao na kuweka utaratibu wa kuingiza vifaa vinavyo hitajika katika msimu wa huzuni za Fatwimiyyu”.

Mmoja wa wahudumu wa kamati ya Mtoto anaenyonya, Sayyid Muntadhiru Jalihawi amesema “Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya wamezowea kuomboleza msiba wa Fatuma Zaharaa (a.s) na kuelezea maisha yake matukufu kwa mazuwaru, katika msimu wa huzuni za Fatwimiyyu kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho ambacho huandaa kila kitu kinachohitajika katika maombolezo hayo ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: