Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imegawa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri.
Kiongozi wa idara Bibi Taghrida Tamimi amesema “Idara ya wahadhiri imegawa zawadi kwa wanafunzi wa Maahadi ya wahadhiri na walimu kwa lengo la kuwashajihisha waendelea kufanya vizuri”.
Akaongeza kuwa “Kunaumuhimu wa kunufaika na wakati katika kuchota elimu na maarifa na kuhakikisha hilo linaonekana katika maisha ya familia, kwa watu kupambika na maadili ya Ahlulbait (a.s) na elimu zao katika kupambana na fikra potofu zinazoingizwa kwenye jamii”.
Akasisitiza kuwa “Kuna umuhimu mkubwa wa kutafuta elimu na kujenga misingi ya kupendana na kuhurumiana katika jamii ya wanawake, akatoa shukrani nyingi kwa watumishi wa shule na uongozi wake”.