Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s)

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili.

Majlisi inafanywa kwa kushirikiana na kituo cha Swidiqatu Twahirah (a.s), inahusisha igizo lenye anuani isemayo (Hujjatul-Kubra) ambalo limeonyesha sehemu ya dhulma aliyofanyiwa Bibi Zaharaa (a.s) na kunyan’ganywa haki yake na maelezo ya kifo chake.

Siku ya mwisho imekuwa na muhadhara wenye anuani isemayo (Dhulma aliyofanyiwa Fatuma baina ya maswali na shubuha), mzungumzaji kataja mambo tofauti ikiwa ni pamoja na, historia ya Zaharaa (a.s), tukio la kushambuliwa nyumba yake, ikahitimishwa kwa kusoma qaswida na tenzi za kuomboleza.

Idara hufanya majlisi za kuomboleza katika maeneo tofauti ya mkoa wa Karbala, kwa lengo la kufundisha historia ya Ahlulbait (a.s) na kulinda misingi ya Dini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: