Mmoja wa watumishi wa idara Sayyid Muntadhiru Dhiyaau-Dini amesema “Idara imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wahadhiri wameongea kuhusu utukufu wa Bibi Zaharaa (a.s) na misingi aliyozingatia katika maisha yake kwenye jamii na ibada”.
Akaongeza kuwa “Majlisi imedumu kwa muda wa siku tatu, wameshiriki wahadhiri na waimbaji wa qaswida, wametaja utukufu wa Bibi Zaharaa (a.s) na historia yake, sambamba na kueleza dhulma alizofanyiwa baada ya kifo cha baba yake (s.a.w.w) na jinsi alivyo pambana kutetea Utume na Uimamu”.
Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) yenye vipengele mbalimbali.









